Wanawake wana uwezo mkubwa wa kupoteza hamu ya kufanya tendo la ngono katika ndoa kulingana na utafiti wa tabia za ngono uliofanywa nchini Uingereza.Utafiti huo umebaini kwamba huku wanawake na wanaume wakionekana kupoteza hamu ya tendo la ngono kutokana na umri wao, wanawake wengi hupoteza hamu hiyo wanapoishi na wapenzi wao kwa muda mrefu.Kwa jumla hali mbaya ya afya mbali na ukosefu wa uhusiano wa kihisia unaathiri hamu ya jinsia zote mbili ya kufanya tendo la ngono.Matokeo hayo yanatokana na mahojiano ya wanaume 5000 na wanawake 6,700 yaliochapishwa na shirika la BMJ Open.Watafiti hao wa Uingereza wamesema kuwa matatizo ya hamu ya ngono yanafaa kutibiwa kwa kumchunguza mtu badala ya kutumia dawa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments